Punguzo la Bei kwa Bidhaa Zetu Sabasaba

Punguzo la Bei kwa Bidhaa Zetu Sabasaba

Kampuni ya Afri Tea & Coffee Blenders (1963) Limited  iliyopata tuzo ya Mshindi wa Kwanza  kwa wazalishaji bora wa bidhaa za ndani katika maonyesho ya 41 ya biashara ya kimataifa   imewashukuru  Watanzania wote kwa  kuendelea kuzipenda, kuzinunua na kutumia bidhaa zao bora,nchini kote na kuwataka kutembelea  banda lao  katika viwanja vya maonyesho Sabasaba.

Akizungumza  na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Masoko na Biashara ya Nje  wa kampuni  hiyo   Ndg. Zachy Mbenna   amesema  mwaka huu wamejipanga  vema kuwahudumia wateja na wameleta  bidhaa  mbalimbali  bora zikiwemo African Pride Tea iliyoboreshwa, Uji Bora Cereal Drink, kahawa ya Africafe 3 in 1, chai ya Green Label iliboreshwa, Maziwa ya Clover yanayodumu kwa muda mrefu na bidhaa za  viungo Vegeta.

“Wateja wetu watakaotembelea katika  banda letu kununua  bidhaa zetu hapa Sabasaba watapata zawadi kemkem na punguzo kubwa la bei. Pia kuna sehemu maalum ambapo mteja wetu  ukifika katika banda letu la maonesho unaweza kuonja bidhaa zetu na kufurahia bidhaa zetu bora. Na ukinunua  bidhaa ya chai na kahawa  utapata zawadi za kikombe na kalamu nzuri za kisasa.” Ndg. Mbenna alisema.

Aidha Mbenna  amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt John  Pombe Magufuli  na Wizara ya viwanda na biashara  , na uongozi wa Tantrade   kwa  kuongeza siku za maonyesho kutoka tarehe 8 hadi 13 imetoa fursa  nyingine kwa watanzania kutembelea maonesho haya ya kimataifa ili kujifunza na kufurahia bidhaa bora kutoka Afri Tea and Coffee Blenders (1963)

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *