Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dk. John Pombe Akitukabidhi Tuzo

Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Dk. John Pombe Akitukabidhi Tuzo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli (katikati) akimkabidhi  Tuzo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Afri Tea and Coffee Blenders (1963) Limited,  Abdulhakim Mulla wakati alipozindua rasmi maonyesho ya biashara maarufu kama sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere. Kulia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mheshimiwa Charles Mwijage akishuhudia tukio hilo.

Kampuni ya Afri Tea & Coffee Blenders (1963) Limited  iliyopata tuzo ya Mshindi wa Kwanza  kwa wazalishaji bora wa bidhaa za ndani katika maonyesho ya 41 ya biashara ya kimataifa   imewashukuru  Watanzania wote kwa  kuendelea kuzipenda, kuzinunua na kutumia bidhaa zao bora popote walipo nchini na kuwataka kutembelea  banda lao  katika viwanja vya maonyesho Sabasaba.

Baada ya kutoa zawadi kwa washindi mbalimbali, Mheshimiwa Rais alitembelea mabanda machache yaliyochaguliwa. Alipotembelea Banda la Afri Tea, Rais Magufuli alitaka kujua kiwanda kinatoa wapi chai yake, swali ambalo Mwenyekiti wa bodi ya Wakurenzi alilijibu kwa ufasaha na kusema kuwa,Tunapata majani ya chai kutoka kwa wakulima wadogo wadogo  wa hapa nchini Tanzania waliopo sehemu mbalimbali kama vile Lupembe-Njombe, Mponde – Tanga, Iringa, Kagera nk.  ‘ Suala la matumizi ya teknolojia na viwanda ili kuongeza thamani ya mazao ya wakulima wa Tanzania ni suala lenye tija kwa Taifa na watu wake pamoja na kuchangia sana katika kutoa fursa ya ukuaji wa uchumi wa mkulima mmojammoja. Kuongeza thamani  ni ajenda muhimu ya utendaji kwa Kampuni ya Afri Tea and Coffee Blenders (1963) Limited.

Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Ndg. Abdulhakim Mulla akiwa pamoja watendaji kutoka ATCB, wa pili kutoka kulia ni Bi Sheila Manafi ambae ni Afisa Mauzo wa ATCB,wa tatu kutoka kushoto ni Bwn.Zachy Mbenna ambaye ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Biashara ya Nje na wa mwisho ni Ndg. Salehe ambae ni Meneja wa  Uzalishaji wa Kahawa wa ATCB wote kwa pamoja wakiifurahia tuzo walizoshinda katika Maonyesho ya Kibiashara ya 41 Saba Saba

 

Akizungumza  na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Masoko na Biashara ya Nje  wa kampuni  hiyo   Ndg. Zachy Mbenna   amesema  mwaka huu wamejipanga  vema kuwahudumia wateja na wameleta  bidhaa  mbalimbali  bora zikiwemo African Pride Tea iliyoboreshwa, Uji Bora Cereal Drink, kahawa ya Africafe 3 in 1, chai ya Green Label iliboreshwa, Maziwa ya Clover yanayodumu kwa muda mrefu na bidhaa za  viungo Vegeta.

“Wateja wetu watakaotembelea katika  banda letu kununua  bidhaa zetu hapa Sabasaba watapata zawadi kemkem na punguzo kubwa la bei. Pia kuna sehemu maalum ambapo mteja wetu  ukifika katika banda letu la maonesho unaweza kuonja bidhaa zetu na kufurahia bidhaa zetu bora. Na ukinunua  bidhaa ya chai na kahawa  utapata zawadi za kikombe na kalamu nzuri za kisasa.” Ndg. Mbenna alisema.

Aidha Mbenna  amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Dkt John  Pombe Magufuli  na Wizara ya viwanda na biashara  , na uongozi wa Tantrade   kwa  kuongeza siku za maonyesho kutoka tarehe 8 hadi 13 imetoa fursa  nyingine kwa watanzania kutembelea maonesho haya ya kimataifa ili kujifunza na kufurahia bidhaa bora kutoka Afri Tea and Coffee Blenders (1963) Limited.

Haya ni maziwa aina ya  Clover ambayo ni moja ya bidhaa inayouzwa na kampuni ya Afri Tea & Coffee Blenders (1963) Limited na inapatikana hapahapa katika vwanja vya maonesho ya Sabasaba

Hizi ni baadhi ya bidhaa za Vegeta, hivi ni viungo maalumu vya chakula kama nyama, samaki, maharage na mboga za majani. Utaweza kujaribu bidhaa hizi zote BURE KABISA ukifika katika banda la AFRI TEA AND COFFEE BLENDERS (1963) LTD lililopo katika viwanja vya Maonyesho ya Sabasaba

UJI BORA Instant Cereal Drink, Hii ni bidhaa ya kipekee kabisa kwa ajili ya watu wote, wakubwa kwa wadogo inayokuwezesha kutengenezea uji mtamu wenye virutubisho vyote vya afya na madini ya Kalsium. Unakuwa tayari ndani ya dakika mbili tu na unakuwa upo tayari kwa matumizi. Ni mzuri sana kwa watu walio busy, watoto wasiopenda kula na wale wenye upungufu wa madini ya Kalsium mwilini

Share this post

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *